28 C
Dar es Salaam
Monday, January 24, 2022

Saa mbili za Halima Mdee mbele ya Kamati ya Bunge

Ramadhan Hassan, Dodoma

Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, amemaliza kuhojiwa na Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili, Kinga na Madaraka ya Bunge kwa kutumia saa mbili.

Mdee amehojiwa leo Jumanne Januari 22 na kamati hiyo, kutokana na hatua ya kuunga mkono kauli ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad kuwa bunge ni dhaifu.

Mdee ambaye aliingia saa 5.03 asubuhi alikuwa akitoka mara kwa mara ndani ya chumba hicho ili kutoa nafasi kwa wajumbe wa kamati hiyo kujadili na kisha kumuita tena na kumuuliza maswali mengine.

Mara ya kwanza alitoka saa 6.40 mchana ambapo alirudi tena saa 6.57 na alipoingia tena alitoka saa 7.28 mchana na kisha kuondoka.

Mdee anahojiwa leo na kamati hiyo wakati CAG akihojiwa jana na kamati hiyo kwa kutumia saa tatu.

Profesa Assad, anadaiwa kutoa kauli kuwa Bunge ni dhaifu wakati akihojiwa na Radio ya Umoja wa Mataifa nchini Marekani na Mdee kuunga mkono kauli hiyo.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
176,379FollowersFollow
531,000SubscribersSubscribe

Latest Articles