28.6 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

Rwanda yazindua simu zake

Kigali, Rwanda

KAMPUNI ya Mara nchini Rwanda imezindua simu mbili za smartphone, ikitaja kuwa za kwanza kutengenezwa barani Afrika.

Hatua hiyo inachochea maono ya nchi hiyo ya kuwa bingwa wa teknolojia katika ukanda wa Afrika.

Simu hizo kwa jina la Mara X na Mara Z zitatumia mfumo wa Google wa Android na kugharimu Dola za Marekani 190 na 130.

Zitashindana na simu za Kampuni ya Samsung ambazo zinauzwa kwa dola 54 huku simu nyingine zisizo na nembo zikiuzwa kwa dola 37.

Kwa mujibu wa Reuters, Ofisa Mkuu Mtendaji wa Kampuni ya Mara, Ashish Thakkar, anawalenga wateja walio tayari kulipa zaidi kwa bidhaa za hali ya juu.

“Hii ni aina ya kwanza ya simu ya smartphone barani Afrika.

“Kampuni hununua na kuunganisha vifaa vya simu nchini Misri, Ethiopia, Algeria na Afrika Kusini. Sisi ni wa kwanza kutengeneza vifaa hivyo hapa Afrika.

“Tunatengeza bodi muhimu ya tarakilishi ya simu hizo (motherboards) mbali na bodi ndogo (sub boards) za simu hizo wakati wa mchakato wote,” alisema Thakkar katika mazungumzo yake na Reuters baada ya kutembelea kampuni hiyo akiandamana na Rais wa Rwanda, Paul Kagame.

Thakkar alisema kiwanda hicho kimegharimu dola milioni 24 na kinaweza kutengeneza simu 1,200 kwa siku.

“Kampuni ya Mara inalenga kujipatia faida kutokana na makubaliano ya biashara huru katika bara hili, mwafaka unaolenga kujenga umoja wa mataifa 55 wa kibiashara ili kupiga jeki mauzo kote barani Afrika,” alisema Thakkar.

Kulingana na Reuters, makubaliano hayo yanatarajiwa kuanza kutekelezwa Julai mwakani, yakilenga kuunganisha takriban watu bilioni 1.3.

Lakini mradi huo upo katika awamu za kwanza hivyo hakuna muda uliotolewa kufutilia mbali kodi.

Kagame alisema kwamba anatumaini simu hizo zitaongeza matumizi ya simu aina ya smartphone miongoni mwa raia wa Rwanda yaliyo asilimia 15 kwa sasa.

“Raia wa Rwanda tayari wanatumia simu aina ya smartphone, lakini tunataka wengi watumie. Uzinduzi wa simu za Mara zitawafanya raia wengi wa Rwanda kumiliki simu zaidi ya aina hizo,” alisema Kagame.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles