30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Rwanda yatangaza ‘lockdown’ kudhibiti maambukizi

Kigali, Rwanda

RWANDA imetangaza kufunga mipaka yote ya nchi hiyo na watu kuamrishwa kusalia majumbani mwao katika juhudi za kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona.

Hatua zingine zilizochukuliwa ni pamoja na watumishi wote wa Serikali na wa sekta binafsi kufanyia kazi nyumbani na safari za kwenda mikoani kusitishwa kwa wiki mbili kukiwa na uwezekano wa muda huo kuongezwa.

Vilabu vya pombe na maduka yasiyo ya chakula pia yamefungwa huku usafiri wa bodabobda ukisitishwa.

Hatua hiyo inajiri siku moja baada ya Wizara ya Afya ya Rwanda siku ya Jumamosi kutangaza kuwa watu wengine sita wameambukizwa virusi vya corona miongoni mwao mtoto mchanga wa miezi 10.

Maambukizi hayo yanaifanya Rwanda kuwa na idadi ya visa 17 vya maambukizi ya virusi vya corona.

Wananchi waliokuwa na hofu wameonekana wakinunua bidhaa za chakula huku baadhi yao wakihofia hali itakuaje.

Hatua zilizochukuliwa na Rwanda kudhibiti coronavirus ni pamoja na kufungwa kwa shule zote za umma na za kibinafsi, maeneo ya kuabudu na sehemu zote za umma.

Matukio kama vile mikusanyiko ya watu katika maeneo ya michezo na harusini vimeahirishwa na wale waliopoteza wapendwa wao watazikwa kwa namna ya kipekee.

Shirikisho la Sola la Rwanda (Ferwafa), pia limetangaza kwamba michuano yote kwa sasa itafanyika bila kuhudhuriwa na mashabiki katika viwanja vya michezo, huku shirikisho la mpira wa mkono nchini humo likiahirisha michezo yake yote.

Maeneo ya umma na maeneo yote ya utoaji wa huduma yameagizwa kuweka dawa za kunawia mikono kwa ajili ya umma unaotembelea maeneo hayo.

Raia wamehimizwa kukaa nyumbani na kuepuka matembezi yasiyo ya maaana na kunawa mikono mara kwa mara kwa muda wa sekunde 20.

Hakuna abiria atakayeruhusiwa kusimama na kutoa wito kwa watu wa eneo na vikosi vya usalama kusaidia kuhakikisha hatua hizo zinatekelezwa.

Waliopatikana na maambukizi hayo awali wote walikua wametoka katika nchi za ng’ambo hivi karibuni.

Siku ya Jumamosi Wizara ya Afya iliwataja watu sita walioambukizwa kuwa ni mwanamke Mfaransa mwenye umri wa miaka 30 na mtoto wake wa miezi 10. Mume wa mama huyu alikuwa pia amepatikana na virusi siku zilizopita.

Mtoto huyo wa miezi 10 ndiye mtu mwenye umri mdogo zaidi aliyewahi kupatika ana coronavirus nchini Rwanda tangu ilipogundulika nchini humo wiki iliyopita.

Mwingine ni Myanrwanda mwenye umri wa miaka 32 aliyefika nchini Rwanda akitokea  Dubai Machi 19, 2020.

Mwanaume kutoka Sweden waliyefika RwandaMachi  03, 2020 lakini akaonyesha dalili za coronavirus Machi 18, 2020 naye alirekodiwa.

Mwanaume Myarwanda mwenye umri wa miaka 32 ambaye amekua akifanya safari katika mataifa ya kigeni ambaye alipatikana na dalili Machi 18, 2020 na mwingine ni mwanaume Mnyarwanda mwenye umri wa miaka 24 aliyefika Rwanda Machi 19, 2020 kutoka India kupitia Doha – Qatar.

Kwa mujibu wa wizara ya afya nchini humo wagonjwa wote wametengwa na wanaendelea kupata matibabu.

Ilielekezwa kuwa watu wote waliofika nchini Rwanda katika kipindi cha siku 14 zilizopita wanatakiwa kujitenga binafsi kwa siku 14 na kufuata maagizo yaliyotolewa juu ya coronavirus.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles