27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Rwanda yapiga marufuku ndege za Boeing 737 Max

KIGALI, RWANDA

SHIRIKA la usafiri wa ndege la nchini Rwanda, limetoa agizo kwa marubani na kampuni za ndege kutoendesha ndege za Boeing 737 Max 8 ama 9 katika anga ya nchi hiyo.

Uamuzi huo wa Rwanda unamaanisha nchi hiyo imejiunga na mataifa mengine duniani ambayo yamepiga marufuku usafiri wa ndege hizo aina ya Boeing 787 Max 8 na Max 9.

Hii inafuatia ajali ya ndege ya Ethiopia Airlines wiki iliyopita ambapo ilianguka muda mfupi baada ya kupaa kutoka mji mkuu Addis Ababa na kusababisha vifo vya watu 157.

Taarifa zinaeleza kwamba, Rwanda ilikuwa na mipango ya kukodisha ndege mbili za aina hiyo Boeing 737- 800. Hata hivyo, huenda mipango hiyo ikasitishwa kwa muda sasa wakati kukisubiriwa uchunguzi wa chanzo cha ajali ya ndege ya Ethiopia iliyoanguka nje kidogo ya mji mkuu Addis Ababa.

Ndege kama hiyo ya kampuni ya Lion Air, ilianguka kutoka pwani ya Indonesia Oktoba mwaka jana na kusababisha vifo vya watu 189. Katika taarifa rasmi iliyowekwa kwenye mtandao wa twitter ya mkurugenzi mkuu katika shirika hilo la usafiri wa ndege Rwanda, Silas Udahemuka, RCAA limesema kwamba marufuku hiyo imeanza kufanya kazi mara moja.

“Shirika la usafiri wa ndege Rwanda kwa uwezo uliopewa katika kifungu cha 16 cha sheria za usafiri wa ndege nchini inaagiza marubani na kampuni za ndege zinazohudumu ndege za Boeing 737 – 8 Max na Boeing 737 – 9 Max, zisiendeshe usafiri wowote wa ndege hizo katika anga ya Rwanda mara moja,” inasema taarifa hiyo.

Marekani hivi karibuni imesitisha usafiri wa ndege hiyo ya Boeing 737 Max yakiwemo mataifa mengine kama Uingereza, Umoja wa Ulaya, China, India na Australia ambayo yote yameamua kusitisha usafiri wa ndege hizo.

Ndege zote za Boeing 737 Max 8 na 9, zimepigwa marufuku kuhudumu hadi angalau Mei baada ya ajali hiyo ya shirika la ndege la Ethiopia, Shirika la kitaifa la usafiri wa ndege nchini Marekani (FAA).

“Ndege hizo hazitahudumu hadi mfumo wake wa uhudumu uimarishwe na uidhinishwe,” imesema FAA.

Mkasa huo wa ndege nje kidogo ya mji mkuu Addis ulisababisha vifo vya watu 157 kutoka mataifa 35. Ni ajali ya pili ya aina hiyo ya ndege ya 737 Max katika muda wa miezi mitano.

Baadhi ya watu wamegusia ufanano wa mikasa hiyo, huku baadhi ya wataalamu wakitaja data ya satelaiti na ushahidi kutoka eneo la mkasa kuonyesha uhusiano wa ajali ya ndege ya Ethiopia na ile iliyotokea Indonesia ya Lion Air mwaka jana.

Wachunguzi nchini Ufaransa wamepokea jukumu la kisanduku kinachonakili data ya safari hiyo ya ndege maarufu ‘black boxes’ wakijaribu kubaini chanzo cha ajali ya ndege hiyo ya Boeing 737 Max. Huenda ikachukua muda kupata data ya awali, lakini mengi itategemea hali ya kisanduku hicho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles