31.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

RUZUKU YAWAPELEKA CUF MAHAKAMANI

Maalim

Na  MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

VIONGOZI wa Chama cha Wananchi (CUF) wanaomwunga mkono Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad, kinatarajia kwenda mahakamani kufungua kesi ya uchotwaji wa fedha za ruzuku Sh milioni 360, dhidi ya mwenyekiti anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya chama hicho,   viongozi hao wanatarajia kukutana kesho katika  kikao ambacho kitahudhuriwa na wajumbe wa Baraza la Wadhamini wanaomwunga mkono Maalim Seif.

Kikao hicho pia kitahudhuriwa na wanasheria na wakurugenzi ambao kwa pamoja watajadili suala hilo na kutoka na uamuzi wa kwenda mahakamani.

“Unajua huo ni kama utakatishaji wa fedha za umma hivyo basi hatuwezi kukaa kimya ni vema hatua stahiki zikachukuliwa,’’ kilisema chanzo hicho.

Pia kilisema kuwa CUF upande wa Lipumba watafunguliwa kesi kila mmoja kwa uzito wake jinsi alivyoshiriki tukio hilo ambalo wameliita ni wizi wa utakatishaji fedha za umma.

Naye Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Habari Uenezi na Uhusiano na Umma, Mbarara Maharagande, alisema Sh milioni 80 ambazo upande wa Profesa Lipumba unadai zimetolewa, zipo na ni mali ya chama.

Mwenyekiti wa Kamati ya Muda ya Uongozi wa chama hicho asiyetambuliwa na Msajili, Julius Mtatiro, alieleza jinsi fedha hizo zilivyotoroshwa kutoka Hazina hadi katika akaunti ya Wilaya ya Temeke na kuishia akaunti binafsi ya mtu aliyetambulika kama Mhina Masoud Omary, kupitia Tawi la NMB.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles