26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Rungu la FIFA latua Simba

5NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (FIFA), limeipiga faini ya Franc 2,000 za Uswisi (sawa na Sh 4,582,000 za Tanzania) klabu ya Simba baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kupuuza maagizo ya Idara ya Utatuzi wa Migogoro ya shirikisho hilo.

Kamati ya idara hiyo ilipokutana Aprili 20, mwaka huu huko Zurich, Uswisi, ilitumia Franc 500 (sawa na Sh 1,145,500), hivyo Simba pia imeagizwa kuzilipa ikiwa ni gharama za kikao cha kufuatilia utekelezaji wa sakata la mchezaji wao wa zamani, Donald Mosoti Omanua, raia wa Kenya.

Simba imeelezwa kupuuza kumlipa Mosoti kwa wakati tangu mkataba wake uvunjwe.

Mosoti aliyesajiliwa msimu wa 2014/15 na kuachwa, alilalamika FIFA ambayo iliona ana hoja, na hivyo Simba kutakiwa kumlipa dola 29,250 (sawa na Sh milioni 62.8) pamoja na kiasi kingine anachodai ni dola 600 (Sh 1,290,000) zilizobaki katika usajili na kufanya jumla ya Sh milioni 64.2.

Pia Mosoti anamlipa mwanasheria wake Felix Majani dola 2,000 (Sh 4.3 milioni) kwa ajili ya kusimamia kesi hiyo.

Majani ambaye pia ni mmoja wa wanasheria wa FIFA, alifungua kesi katika shirikisho hilo kuwashtaki Simba kwa kukiuka makubaliano ya mkataba na mteja wake.

Kwa kosa hilo, Simba inatakiwa kulipa fedha hizo ndani ya siku 30 kuanzia tarehe ya kupokea barua ya FIFA iliyoandikwa Mei 3, mwaka huu na kufika Tanzania jana.

Katika barua hiyo ambayo TFF ina nakala yake, Simba imepewa amri ya kulipa fedha hizo katika muda uliopangwa – siku 30 kutoka sasa, na isipofanya hivyo itashushwa daraja kutoka Ligi Kuu hadi Ligi Daraja la Kwanza au zaidi.

Kwa upande wake, TFF imeagizwa kusimamia vema utekelezwaji wa maagizo hayo vinginevyo itachukuliwa hatua stahiki ikiwamo kuiondoa Tanzania katika mashindano ya kimataifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles