33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

RUGEMALIRA ATAJA ALIODAI WEZI FEDHA ZA ESCROW

Na Mwandishi Wetu- Dar es Salaam

HATIMAYE mfanyabiashara, James Rugemalira, anayekabiliwa na kesi ya utakatishaji fedha amedai kuwa benki za Standard Chartered ndizo zilizoisababishia Serikali hasara ya Sh trilioni 37.

Rugemalira ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kampuni ya VIP Engineering and Marketing Ltd, alitoa madai hayo baada ya mara kadhaa kuomba kuonana na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ili ampe ushirikiano na kutoa ushahidi wa nani anayepaswa kukamatwa katika kesi hiyo ya utakatishaji wa zaidi ya Sh bilioni 300 zilizohifadhiwa Akaunti ya Tegeta Escrow kwa kuwa anawafahamu.

Rugemalira alitoa madai hayo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, wakati kesi hiyo inayomkabili yeye na mwenzake ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL, Harbinder Sethi, ilipopelekwa kwa ajili ya kutajwa.

“Katika kusaidia upelelezi wa kesi hii kukamilika nimeshataja benki za Standard Chartered Tanzania Limited na Standard Chartered Hong Kong Limited kuwa ndizo zimeisababishia Serikali kupata hasara ya shilingi trilioni 37. Nimeshapeleka ushahidi wote.

“Escrow yote imesababishwa na benki hiyo. Naomba upande wa Jamhuri kuiondoa kesi hiyo chini ya kifungu cha 91 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) na wamkamate Standard Chartered, nikatibiwe ili niwe shahidi wao mzuri nikifa itakuwa tabu,” alidai.

Kabla ya kutoa madai hayo, Rugemalira alidai kwamba ni mgonjwa kwa miaka tisa sasa na hajaenda kutibiwa kwa miezi sita.

“Mwaka mpya uvimbe ulianza tena. Nimetoa taarifa kwa uongozi wa magereza…

Kwa habari zaidi usikose kununua nakala yako

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles