30.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, January 31, 2023

Contact us: [email protected]

Rufaa ya Ole Nangole imekwama kusikilizwa

JOPO la Majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa Tanzania limekwama kusikiliza Rufaa ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Longido,Onesmo Ole Nangole(Chadema) dhidi ya aliyekuwa mgombea ubunge wa CCM, Dkt.Steven Kiruswa, baada ya Mawakili wa Dkt.Kiruswa kuwasilisha pingamizi mbili za kisheria.

Rufaa hiyo namba 129 ya mwaka 2016,ilikuwa isikilizwe mbele ya Jaji Benard Luanda,Jaji musa Kipenka na Jaji Stela Mugasha ambapo Ole Nangole anapinga maamuzi ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha,yaliyomvua ubunge maamuzi yaliyotolewa na Jaji Sivangilwa Mwangesi.

Katika rufaa hiyo Ole Nangole alikuwa akiwakilishwa na Mawakili Method Kimomogoro na John Materu huku Dkt.Kiruswa akiwakilishwa na Mawakili Dkt.Masumbuko Lamwai,Edmund Ngemela na Daudi Haraka na wajibu maombi wa pili na tatu(Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Longido),wakiwakilishwa na Mawakili Juma Ramadhan,David Kakwaya ba Fortunatus Mhalila.

Dkt.Lamwai aliwasilisha pingamizi mbili ambazo ni mapungufu yaliyomo kwenye rekodi ya notisi ya rufaa ikiwemo kuongezeka kwa vitabu na maneno ambapo Novemba 24 mwaka jana wakat rufaa hiyo inaahirishwa mawakili wa Mleta Rufaa waliamriwa kuwaongeza wajibu rufaa wawili(AG na Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Longido) ila wao wameongeza na maneno mengine.

Jaji Luanda aliahirisha rufaa hiyo baada ya kusikiliza hoja za kisheria za pande zote mbili na kusema kuwa wataenda kuzitafakari na tarehe ya kutoa uamuzi iwapo wanakubaliana na pingamizi au lah watatoa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles