25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Rufaa utakatishaji milioni 400/- yatupwa

Pg 2Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imekataa kulifuta shtaka la kutakatisha fedha Sh milioni 400 linalomkabili mtuhumiwa wa wizi wa Sh milioni saba kwa dakika, Mohammedi Mustafa na mwenzake.

Uamuzi wa kukataa kulifuta shtaka hilo ulitolewa jana na Hakimu Mkazi, Wilbard Mashauri baada ya kusikiliza hoja za pande mbili zinazopingana katika kesi hiyo.

Mustafa na Sammuel Lema ambaye ni  Mkurugenzi wa Kampuni ya Northern Engineering Work Limited wanakabiliwa na jumla ya mashtaka 222.

Watuhumiwa hao wanaokabiliwa na kesi ya jinai namba 36 ya 2016, wanadaiwa kutenda makosa kati ya Februari mosi mwaka 2013 na Desemba 31,2015.

Katika hati ya mashtaka,  kwa pamoja wanadaiwa kughushi nyaraka mbalimbali za Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) kuanzia kosa namba mbili hadi 103, kosa namba 104 hadi 142 yakidaiwa kufanywa na mtuhumiwa wa kwanza, Mustafa.

Shtaka la 220 ambalo ni la kukwepa kulipa kodi lilifanywa katika kipindi hicho ambapo mshtakiwa wa kwanza anatuhumiwa kukwepa kodi ya Sh bilioni 14.

Shtaka la 221 linalohusu utakatishaji fedha linadaiwa kutendwa na washtakiwa wote wawili, inadaiwa Sh milioni 400 zilitakatishwa kupitia akaunti ya Iqbal Jafareri katika Benki ya IMM tawi la Kariakoo.

Shtaka la mwisho ni kuisababishia TRA hasara ya Sh bilioni 13  kupitia ukwepaji kodi.

Wakili Alex Mgongolwa na wenzake wa upande wa utetezi waliwasilisha hoja kupinga shtaka la 221 la utakatishaji fedha kwa madai kuwa lina upungufu kisheria ambao hauwezi kurekebishika na kwamba maelezo ya shtaka hilo hayajitoshelezi.

Wakili wa Serikali Mkuu, Mutalemwa alipinga hoja hizo kwa madai kwamba mahakama haina mamlaka ya kutoa uamuzi huo.

Akitoa uamuzi, Hakimu Mashauri alisema mahakama ilisikiliza hoja za pande zote mbili na katika kufikia uamuzi ilijikita kuangalia mamlaka ya mahakama kuangalia uhalali wa hati ya mashtaka.

Alisema katika kutetea hoja zilizowasilishwa kesi mbalimbali za mahakama ya juu na moja wapo ilishakatiwa rufaa hivyo haiwezi kutumika katika kufikia uamuzi.

“Kesi iliyopo mahakamani inatakiwa kusikilizwa Mahakama Kuu, inapitia katika mahakama ya chini kwa ajili yua kusubiria upelelezi kukamilika ihamie mahakama hiyo ya juu.

“Kwa kuzingatia mipaka hiyo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kulifuta shtaka hilo la kutakatisha fedha,”alisema hakimu na kuyatupa maombi ya upande wa utetezi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles