21.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, August 16, 2022

RPC Shana aanza na wauza dawa za kulevya

NA ELIYA MBONEA-ARUSHA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha (RPC), Jonathan Shana amewataka wamiliki wa vijiwe vya kuuzia dawa za kulevya ikiwamo Mirungi na Bangi kuvivunja haraka.

Kauli hiyo ameitoa mjini Arusha leo, Machi 19 mbele ya wanahabari alipokuwa akitangaza vipaumbele na mikakati yake ya kazi baada ya kuhamishiwa mkoani hapa akitokea Mkoa wa Mwanza.

“Adui yangu ni mhalifu sintakuwa na salia mtume kwa mhalifu nikikupiga napiga kweli, nimeletwa Arusha kulinda raia na mali zao. Huu ni mji wa Kitalii, niwahakikishie watakuwa salama.

“Natoa onyo kwa wahalifu wote wakiwamo wanaotumia silaha mimi nitatumia silaha nzito zaidi yao, dawa ya moto ni moto kwangu hakuna mhalifu mdogo, wote ni wahalifu,” amesema RPC Shana.

“Nikimaliza kuzungumza hapa moto wangu utaanza kuonekana huko mitaani, wale wenye vijiwe na mabaraza ya kuuza mirundi waanze kuvunja wenyewe,” alisema RPC Shana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,814FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles