30.2 C
Dar es Salaam
Sunday, March 26, 2023

Contact us: [email protected]

RPC: Bodaboda wameanza kujitambua

Fatuma Said Na Yohana Paul -Mwanza

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Murilo amesema  vijana wanaondesha pikipiki mkoani humo,  wamejitambua  na  kuachana na uhalifu na hivi sasa wanafanya shughuli hiyo kama ajira yao rasmi.

Pia amewametajwa kama kundi linaloongoza kwa kuchangia damu kwa asilimia 60.

Kamanda Murilo, alitoa kauli hiyo jana wakati akiwaongoza  bodaboda kujitolea kuchangia damu kwa ajili  kuwasaidia majeruhiwa wa ajali ya lori la mafuta iliyotokea  mkoani Morogoro hivi karibuni.

Aliwashukuru waendesha pikipiki kwa kutambua umuhimu wa kuchangia damu kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa waliolazwa  hospitali za  Morogoro na Muhimbili, Dar es Salaam, wakipatiwa matibabu.

“Tulikuwa tukifanya operesheni ya kuwatafuta wahalifu wa matukio mbalimbali,watu watano kati  10 tunaowakamata ni waendesha pikipiki, mlikuwa mnashirikiana na majambazi kufanya vitendo vya kuvunja sheria lakini leo mmekuwa watakatifu na watu wa Mungu.

“Leo hii polisi tunashukuru bodaboda wamejitambua na kuachana kabisa kujihusisha na uhalifu, nyinyi ndio mnatusaidia kuwatambua maana mnawabeba,tunatoa shukrani nyingi.

“Naomba muendelee na moyo wa kujitolea kuchangia damu, muwe mabalozi kwa jeshi la polisi mkiona mtu ambaye mnatilia shaka, toeni taarifa haraka kwetu, polisi tupo macho muda wote, isitoshe namba yangu inapatikana ukipiga tuna napokea,”alisema.

Kwa upande wa Mratibu wa Maabara na Damu Salama  Mkoa wa Mwanza, Julius Shigella aliwashukuru bodaboda kwa kujitolea na kufafanikisha kupata chupa za damu 120.

Alisema vituo mbalimbali vilivyowekwa maeneo kadhaa ya mkoa huo, bodaboda ndio  wanaongoza kuchangia damu, hivyo aliwataka kuendelea na moyo huo kwani kwa hospitali zote zinahitaji chupa 80 kwa siku kwa ajili ya wagonjwa.

“Mahitaji ya mkoa ni chupa 80 kwa siku,kwa mwezi zinahitajika  chupa 2, 400, zinazopatikana ni asilimia  60 pekee  na upungufu ni asilimia 40.

“Ukiwa umechangia damu mara kadhaa unakuwa na kadi fulani tunakupatia na ukiwa na mgonjwa wako anahitaji huduma hiyo, huwezi kusumbuka, tahudumia haraka, nawaomba Watanzania wawe na utamaduni wa kujitolea damu,”alisema.

Naye Mwenyekiti wa Bodaboda Mkoa wa Mwanza, Gerald Nyerembe, alisema wanajitolea kutokana na kuguiswa na tukio la ajali ya Morogoro.

Alimshukuru Kamanda Murilo kwa kitendo cha kufanya operesheni ya kutafuta pikipiki zilizoibiwa na kupelekwa mikoa mingine na kuzirejesha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,195FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles