27.7 C
Dar es Salaam
Saturday, June 10, 2023

Contact us: [email protected]

Roy Hodgson apata ofa China

Roy Hodgson
Roy Hodgson

LONDON, ENGLAND

ALIYEKUWA kocha wa timu ya taifa ya England, Roy Hodgson, amepata ofa ya kufundisha klabu nchini China mara baada ya kujiuzulu katika timu hiyo ya taifa.

Hodgson mwenye umri wa miaka 68, alichukua maamuzi ya kujiuzulu kutokana na kutolewa kwenye Kombe la Euro 2016 hatua ya 16 bora dhidi ya Iceland kwa mabao 2-1.

Mtendaji Mkuu wa michezo nchini China, Eric Gao, ameweka wazi kwamba kuna ofa nyingi ameandaliwa kocha huyo kutokana na kutambua uwezo wake.

“Klabu ambazo zinashiriki Ligi Kuu nchini China, zinapenda kuwa na makocha ambao wana uwezo mkubwa duniani, kuna klabu nyingi tayari zimeonesha nia ya kumtaka kocha huyo na wametangaza ofa zao.

“Ninaamini kocha huyo atakuja kunufaika na fedha kutokana na uwezo wake pamoja na wasifu wake ambao unapendwa na ligi hiyo.

“Ligi ya China inahitaji mabadiliko makubwa, hivyo wanatakiwa wawekezaji kujitokeza kwa wingi kuweza kulisogeza soka hilo mbali,” alisema Gao.

Hata hivyo, tayari timu ya taifa ya England imeweka wazi kwamba inatarajia kumtangaza Gareth Southgate, kuwa kocha wa muda ambaye anachukua nafasi ya Hodgson hadi pale atakapopatikana kocha mpya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,414FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles