26.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 6, 2023

Contact us: [email protected]

Rose ndauka ageukia Bongo fleva

Brighiter Masaki, Dar es salaam

Mrembo kutoka tasnia ya Filamu nchini, Rose Ndauka, amefunguka kuingia rasmi kwenye tasnia ya muziki wa hip hop huku akitamani kufanya kazi na msanii G nako na Rose Lee.

Akizungumza na Mtanzania Digital, mapema leo Aprili 8 masaki jijini Dar essalaam wakati akiachia wimbo wake, Rose amesema kuwa anakipaji cha kuimba na kuchana muda mrefu.

“Nilikuwa nasubili muda ufike niweze kuachia kazi zangu nilizoweza kufanya, nina nyimbo zaidi ya saba ila nimeamua kuanza na hii moja lakini kazi zitaendelea” amesema Rose

Aidha ameongeza kuwa anatamani sana kuja kufanyakazi na G Nako pamoja na Rose Lee kwa kuwa wanafanya muziki kama anaoufanya yeye.

“Nina vipaji vingi, kuigiza kuimba na uongozi ni kiongozi mzuri sana usishangae Siku moja ukiniona kwenye siasa hakuna kinachonishinda kabisa na ndoto hizo ninazo” amesema Rose

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles