27.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 5, 2023

Contact us: [email protected]

Rooney kuiongezea nguvu Man United

Rooney_1711416aMANCHESTER, UNITED

NAHODHA wa klabu ya Manchester United, Wayne Rooney, anatarajia kuungana na klabu hiyo kwa ajili ya kuiongezea nguvu katika mchezo wa Ligi Kuu nchini England baada ya kukaa nje ya uwanja kutokana na kusumbuliwa na enka.

Mchezaji huyo kwa sasa yupo vizuri na ataungana na wachezaji wenzake kwa ajili ya mchezo huo dhidi ya Norwich, kesho kwenye Uwanja wa Old Trafford.

Nyota huyo alipata majeraha hayo mwezi uliopita katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Leicester City, ambapo timu hizo zilitoka sare ya 1-1, pia aliukosa mchezo wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya dhidi ya Wolfsburg ambapo United ilitupwa nje ya michuano hiyo.

Kocha wa Manchester United, Van Gaal, anaamini ujio wa mchezaji huyo utakuwa na manufaa makubwa, hasa katika safu ya ushambuliaji japokuwa alikuwa majeruhi, lakini atashirikiana na Anthony Martial ambaye naye alikuwa majeruhi lakini kwa sasa yupo fiti.

“Tumekuwa na kipindi kigumu kutokana na kuwakosa baadhi ya wachezaji ambao walikuwa majeruhi, lakini kwa sasa ninaamini tutafanya vizuri kutokana na ujio wa Rooney, tunatakiwa kushinda katika michezo yetu ijayo ili kujiweka pazuri katika msimamo wa Ligi,” alisema Van Gaal.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles