29.7 C
Dar es Salaam
Friday, October 4, 2024

Contact us: [email protected]

Rooney amkingia kifua Van Gaal

Wayne-RooneyMANCHESTER, ENGLAND

NAHODHA wa klabu ya Manchester United, Wayne Rooney, amedai kwamba wachezaji wanapaswa kulaumiwa na sio kocha wao, Van Gaal.

Mshambuliaji huyo amesisitiza kwamba, wachezaji hawachezi kulingana na majukumu yao hivyo lawama anatupiwa kocha badala yao ambao wanatakiwa kuonesha uwezo wao kwa lengo la kuitetea klabu.

Mwishoni mwa wiki iliyopita timu hiyo ilishuka dimbani katika mchezo wa Kombe la FA na kufanikiwa kushinda mabao 3-1 dhidi ya wapinzani wao Derby County.

Kutokana na ushindi huo, Rooney anaamini kuwa wachezaji wanatakiwa kuwajibika kama timu ina shida au kufungwa na sio kocha wa kutupiwa lawama.

“Sio vizuri lawama kutupiwa kocha pale timu inapopoteza mchezo wake, sisi wachezaji tunakuwa uwanjani hivyo tunatakiwa kuonesha majukumu yetu ili kuweza kuibeba timu.

“Najua kila mchezaji anaingia uwanjani kwa ajili ya kutafuta ushindi, lakini kama hachezi kufuatana na majukumu yake basi timu haiwezi kushinda kisha kosa linakuja kuwa la kocha badala ya wachezaji,” alisema Rooney.

Hata hivyo, kocha wa klabu hiyo, Van Gaal, anaamini kuwa watafanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano hiyo ya Kombe la FA msimu huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles