29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

Rooney amkingia kifua Depay

Wayne-Rooney-601018MANCHESTER, ENGLAND

NAHODHA wa timu ya Manchester United, Wayne Rooney, amesema hakuna sababu ya kumtupia lawama mshambuliaji wake, Memphis Depay, kwa makosa aliyoyafanya katika mchezo dhidi ya Chelsea mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Stamford Bridge.

Katika mchezo ambao ulimalizika kwa sare ya 1-1, mshambuliaji huyo alionekana kucheza chini ya kiwango huku akichelewa kutoa pasi ya wazi kwa kiungo wake, Morgan Schneiderlin na kuwafanya wachelewe kupata ushindi katika mchezo huo.

Hata hivyo, Rooney amedai kwamba hakuna sababu ya kumtupia lawama mshambuliaji huyo, ila klabu yote kwa ujumla imecheza chini ya kiwango.

“Nadhani hakuna ambaye ameyafurahia matokeo dhidi ya Chelsea, haya ni makosa yetu sote na sio kumuangalia mtu mmoja, najua wengi wanamtupia lawama Depay, lakini ukweli ni kwamba wote tumefanya makosa, ushirikiano ulikuwa mdogo na ndiyo maana mambo yakawa tofauti.

“Depay ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa bila ya kujali kilichotokea, ila wote kwa ujumla tulicheza chini ya kiwango hata pasi zilikuwa hazionekani,” alisema Rooney.

Hata hivyo, Rooney amemsifia mlinda mlango wao, De Gea, kwa uwezo aliouonesha katika mchezo huo kwa kuokoa mipira mingi ya hatari ambapo bila hivyo wangekuwa kwenye wakati mgumu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles