25.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 29, 2022

Contact us: [email protected]

Ronaldo: Mboga za majani tiba ya Corona

TURIN, Italia

STAA wa Juventus, Cristiano Ronaldo, amewataka mashabiki wake ‘kuvipiga’ virusi vya Corona kwa kula mboga za majani na kutenga muda wa kukaa juani.

Ifahamike kuwa ushahuri wake huo alioutoa kupitia akaunti yake ya mtandao wa Instagam umekuja baada ya taarifa za hivi karibuni kuripoti amepata maambukizi.

Akitoa ushahuri wa namna ya kukabiliana na Corona, CR7 alisema: “Kukaa juani inasaidia sana, watu hawajui tu. Ninapopata nafasi, huwa naoga juani. 

“Kwa hapa Turin, ni ngumu kidogo (kupata jua) lakini huwa najaribu kupata walau dakika 20 au 30…” 

Huku akigusia umuhimu wa kulala vizuri, Ronaldo alizungumzia hilo la mboga za majani, akisema: “Unatakiwa kula vizuri, ule sana mboga za majani…”

Katika hatua nyingine, Ronaldo alikanusha taarifa zilizodai alivunja sheria inayomtaka mwathirika wa virusi hivyo kujitenga kwa kukaa ndani.

Akijibu shutuma hizo, alisema si kweli na badala yake anaishi kwenye eneo la peke yake, tofauti na vyumba vinavyotumiwa na familia yake.

Akisisitiza kuwa hali hiyo ya kukaa mbali na familia yake inamtesa, alikiri hakuna namna ya kuwakinga watu wake na ugonjwa wa Corona zaidi ya kufanya hivyo.

Wakati huo huo, imeripotiwa kuwa klabu yake ya Juventus imepanga kumpiga bei pindi tu dirisha kubwa la usajili litakapofunguliwa hapo mwakani.

Juu ya uamuzi huo, ni katika mpango wa mabosi wa Juventus kupunguza mzigo mzito wa mshahara mnono anaolipwa mchezaji huyo waliyemng’oa Real Madrid mwaka juzi.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,444FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles