26.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 8, 2024

Contact us: [email protected]

RONALDO HATIHATI KUIKOSA MICHEZO 12 LA LIGA

BARCELONA, HISPANIA

MSHAMBULIAJI wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo, huenda akafungiwa michezo minne au 12 endapo atakutwa na hatia ya kumsukuma mwamuzi, Ricardo De Burgos, katika mchezo dhidi ya Barcelona.

Kwenye mchezo huo wa Super Cup ya Hispania uliochezwa Uwanja wa Nou Camp, Madrid ilishinda mabao 3-1 huku Ronaldo akitolewa nje kwa kuoneshwa kadi nyekundu.

Kwa mujibu wa sheria za soka la Hispania, mchezaji anaweza kufungiwa kuanzia michezo minne hadi 12 ikithibitika amemsukuma mwamuzi.

Kifungu cha 96 cha sheria ya soka la Hispania, kinasema kuwa mchezaji akimsukuma, kumtingisha, kumbeba mwamuzi katika hali ya kuashiria vurugu atafungiwa michezo minne au 12.

Ronaldo, aliyeingia kama mchezaji wa akiba, alirejesha Real Madrid mbele alipokimbia kutoka katikati ya uwanja na kufunga, lakini alipewa kadi ya njano kwa kuvua shati lake akiwa anashangilia bao lake.

Muda mfupi baadaye, alioneshwa kadi nyingine ya njano kwa kujiangusha na akaondolewa uwanjani kwa kuoneshwa kadi nyekundu.

Mshindi huyo wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia, aliamini kwamba alitakiwa kupewa penalti baada ya kuanguka alipokabiliwa na Samuel Umtiti na alionekana kumsukuma mwamuzi baada kuoneshwa kadi nyekundu.

Katika mchezo huo beki wa Barcelona, Gerard Pique, alijifunga kupitia krosi iliyochongwa na Marcelo Junior, kabla ya Lionel Messi kusawazisha kupitia mkwaju wa penalti.

Barcelona walionekana kutatizika bila Neymar ambaye amehamia timu ya  Paris Saint Germain (PSG) kwa rekodi ya dunia ya pauni milioni 200.

Madrid wanatarajia kuwa wenyeji wa Barcelona katika mechi ya marudiano itakayochezwa kesho saa 6:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Barcelona walimchezesha Gerard Deulofeu safu ya ushambuliaji pamoja na Lionel Messi na Luis Suarez.

Katika ripoti ya mwamuzi huyo alidai kwamba alisukumwa na Ronaldo baada ya kuoneshwa kadi nyekundu kitendo ambacho kiliashiria hakukubaliana na hatua hiyo.

Kitendo kama hicho kilitokea Aprili mwaka huu kwa mshambuliaji wa Las Palmas, Marko Livaja, ambaye alifungiwa michezo mitano, mchezo mmoja wa kadi nyekundu na minne kama adhabu.

Adhabu aliyopata Livaja ilitokana na sheria ya Ligi ya La Liga  ambapo kutokana na kutodhamiria kitendo hicho aliadhibiwa  kifungo cha michezo minne

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles