21.2 C
Dar es Salaam
Saturday, August 13, 2022

Ronaldo hataki kukutana Real Madrid

TURIN, ITALIA

MSHAMBULIAJI wa timu ya Juventus, Cristiano Ronaldo, ameweka wazi kuwa hataki kukutana na timu yake ya zamani Real Madrid kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 bora.


Juventus wamemaliza nafasi ya kwanza kwenye kundi la A, huku Real Madrid wao wakimaliza nafasi ya pili kwenye kundi A, hivyo dro ya hatua ya 16 bora inatarajiwa kupangwa Jumatatu wiki ijayo.


Timu ambazo zimemaliza hatua ya makundi zikishika nafasi ya kwanza zinachezeshwa dro dhidi ya zile zilizomaliza nafasi ya pili, hivyo Ronaldo amedai anahofia kupangiwa na timu yake hiyo ya zamani kwenye 16 bora.
Amedai hatokuwa na furaha endapo atakutana na timu hiyo, lakini atafurahi kama atakuja kukutana kwenye mchezo wa fainali huko Uturuki, Mei mwakani.


Ronaldo kabla ya kujiunga Juventus alikuwa anakipiga katika klabu ya Real Madrid tangu mwaka 2009 na kuondoka wakati wa kiangazi mwaka jana na kujiunga na Juventus.


“Real Madrid ni timu bora duniani, lakini kwa sasa sipendi kukutana nao kwa kuwa itakuwa mapema sana, nimeondoka hapo hivi karibuni, hivyo kukutana nao tena siku za hivi karibuni itakuwa ngumu kwangu.


“Bado ninawakumbuka wachezaji ambao nimekuwa nao kwa kipindi kirefu ndani ya kikosi hicho, hivyo ni vizuri nikaja kukutana nao kwenye mchezo wa fainali kwa kuwa itakuwa haina nanma, ila kwa sasa itaniumiza sana,” alisema Ronaldo.


Hata hivyo Ronaldo msimu huu bado hajaonekana kuwa kwenye kiwango kizuri kama wakati anakipiga ndani ya klabu ya Real Madrid.

Katika michezo kadhaa iliopita mchezaji huyo amekuwa akitolewa kabla ya mchezo kumalizika jambo ambalo lilikuwa limeacha maswali mengi kwa mashabiki.


Kocha wa timu hiyo Maurizio Sarri, aliwahi kuweka wazi kuwa amekuwa akimtoa mchezaji huyo kwenye baadhi ya michezo kutokana na kutokuwa fiti pamoja na kuwa majeruhi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,590FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles