23.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 27, 2021

RONALDO: BADO YUPO MWENYE WASIWASI NA MIMI?

MUNICH, UJERUMANI


BAADA ya mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Real Madrid, kushinda mabao 2-1 dhidi ya Bayern Munich, staa wa timu hiyo, Cristiano Ronaldo, ameuliza kama bado kuna mtu mwenye wasiwasi juu ya kiwango chake.

Katika mchezo huo Ronaldo alipeleka kilio kwa mashabiki wa Bayern Munich baada ya kufunga mabao yote mawili, huku bao la Bayern Munich likiwekwa wavuni na kiungo mshambuliaji, Arturo Vidal.

Hata hivyo, kiungo huyo alishindwa kuibeba timu yake baada ya kukosa bao kwa mkwaju wa penalti ambapo mashabiki wa klabu hiyo walishangaa kutokana na kupaisha kwake, huku kwenye mitandao ya kijamii wakidai penalti hiyo ilipaa kama Rocket.

Mabao ya Ronaldo yamemfanya aweke historia mpya ya kufikisha mabao 100 katika michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Lakini katika michezo ya hivi karibuni mshambuliaji huyo amekuwa na ukame wa mabao na kuwapa wasiwasi mashabiki juu ya kiwango chake, ila mabao hayo yamempa swali kwa mashabiki hao.

“Kuna mtu yeyote ambaye bado ana swali juu ya kiwango changu? Nadhani kila kitu kimejionesha ila ninaamini bado wapo ambao wana wasiwasi na mimi huku wakidai kiwango kimeshuka.

“Kwa wale ambao wapo karibu sana na mimi ni wazi kwamba wala hawana shaka, wanaona kazi ninayoifanya na kukubali, ila huwezi kukubalika na wote hata kama unafanya vizuri.

“Soka ni mchezo ambao hautabiriki, kuna mambo mbalimbali yanaweza kutokea bila ya kutarajia na kuwashtua mashabiki na wadau wa soka, katika mchezo dhidi ya Bayern ulikuwa na mambo kama hayo.

“Tumefanikiwa kushinda lakini wao walijikuta wakiwa pungufu baada ya mchezaji wao kuoneshwa kadi nyekundu, haikuwa kazi rahisi kucheza na timu kubwa kama Bayern Munich ambayo inaongoza kisha kufanikiwa kusawazisha na kuongeza bao.

“Kwa sasa naweza kusema tumejiweka katika mazingira mazuri ya kuendelea kusonga mbele endapo tutafanya hivyo kwenye uwanja wa nyumbani Santiago Bernabeu, lakini kama Vidal angeweza kufunga penalti yake mchezo ungezidi kuwa mgumu sana,” alisema Ronaldo.

Michezo mingine ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya ni pamoja na Borussia Dortmund ambayo ilikubali kichapo kwenye uwanja wa nyumbani cha mabao 3-2 dhidi ya Monacco, wakati huo Atletico Madrid wakiwa nyumbani walishinda bao 1-0 dhidi ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu nchini England, Leicester City.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
163,319FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles