LISBON, Ureno
JANA Cristiano Ronaldo alifunga mara tatu wakati timu yake ya taifa ya Ureno ikiifunga Luxembourg mabao 5-0 na hiyo inamfanya straika huyo kuwa mchezaji pekee aliyefunga ‘hat trick’ 10 akiwa na timu ya taifa.
Katika mchezo huo wa kufuzu fainali za Kombe la Dunia za mwakani, Ronaldo alipachika mawili kwa mikwaju ya penalti ndani ya dakika 13 za mwanzo, kabla ya kumalizia la tatu katika dakika ya 87.
Kwa upande mwingine, anahitaji kuifungia Ureno mabao matatu tu ili awe mchezaji aliyefunga mabao mara nyingi katika historia ya mechi za kufuzu michuano hiyo.
Carlos Ruiz raia wa Guatemala ndiye anayeshikilia rekodi hiyo kwani aliingia kambani mara 39 akilichezea taifa hilo kuanzia mwaka 1998 hadi 2016.