25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 28, 2023

Contact us: [email protected]

Ronaldo awapa matatizo Man United

MANCHESTER,ENGLAND

HATIMAYE timu ya Manchester United imepigwa faini ya pauni 7,000, ambazo ni zaidi ya milioni 20 za Kitanzania kutokana na baadhi ya mashabiki kuingia uwanjani kumkumbatia nyota wa Juventus, Cristiano Ronaldo.

Manchester United walishuka dimbani dhidi ya Juventus mwishoni mwa mwezi uliopita katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, huku Manchester United wakikubali kichapo cha bao 1-0 kwenye uwanja wa nyumbani lililowekwa wavuni na Paolo Dybala.

Ronaldo aliwahi kuwa mmoja kati ya wachezaji wa Manchester United walioipa heshima kubwa klabu hiyo kuanzia mwaka 2003 hadi 2009.

Katika mchezo huo, mashabiki wa Manchester United, walijisikia kuwa na furaha kubwa kumuona mchezaji wao huyo wa zamani akitua ndani ya Old Trafford akiwa na klabu yake mpya ya Juventus.

Hata hivyo, mmoja kati ya mashabiki hao alionekana kwenda na simu yake uwanjani kwa ajili ya kwenda kupiga naye picha.

Baada ya uchunguzi, shabiki mmoja kati ya watatu hao alionekana kuwa na bastola mbili, lakini zilikuwa feki.

Kutokana na kitendo hicho cha mashabiki watatu kuingia uwanjani, chama cha soka barani Ulaya, UEFA, juzi kilitangaza kwamba Manchester United lazima walipe faini ya pauni 7,000 kutokana na kitendo cha kuwasumbua walinzi wa uwanjani.

Hii si mara ya kwanza kwa Manchester United kupigwa rungu la faini kutoka kwa Uefa, mapema mwezi uliopita, walipigwa faini ya pauni 13,000, zaidi ya milioni 38 za Kitanzania kutokana na kuchelewesha mchezo wao dhidi ya Valencia kwenye uwanja huo wa nyumbani.

Hata hivyo, Manchester United wenyewe wameweka wazi kuwa, watafanya uchunguzi kwa walinzi ambao walisababisha mashabiki hao kuingia uwanjani, ikiwezekana wachukuliwe hatua.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,224FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles