Ronaldo amlilia baba yake

0
1243

Turin, Italia

MSHAMBULIAJI wa timu ya Juventus, Cristiano Ronaldo, mwishoni mwa wiki iliopita alijikuta akitokwa na machozi baada ya kuoneshwa video ya marehemu baba yake wakati akimtabiria makubwa katika maisha yake ya soka.

Baba wa Ronaldo alipoteza maisha mwaka 2005 baada ya Ini kushindwa kufanya kazi kutokana na kunywa pombe kali kupita kiasi. Lakini kabla ya kifo chake aliwahi kusema Ronaldo atakuja kuwa mmoja kati ya wachezaji bora duniani, lakini Ronaldo hakuwahi kuyasikia maneno hayo ya baba yake alipooneshwa mwishoni mwa wiki wakati wa mahojiano na Piers Morgan.

“Sijawahi kuiona video hii, wala sikutarajia kuna video kama hii, hata siamini, alisema Ronaldo huku akilia mara baada ya kuoneshwa video hiyo ya baba yake ambaye aliongea maneno hayo mara baada ya kumalizika kwa michuano ya Euro 2004, mchezaji huyo akiwa anaitumikia timu ya taifa Ureno.

“Nadhani haya mahojiano yalikuwa mazuri sana, lakini kwa upande wangu sikutarajia kama ningeweza kulia baada ya kuiona picha ya baba, naomba niichukue kwa ajili ya kwenda kuionesha familia yangu.

“Ukweli ni kwamba sikuwahi kumjua baba yangu kwa asilimia 100, nakumbuka alikuwa mlevi, hivyo ilikuwa ngumu kupata muda wa kuzungumza naye mara kwa mara.

“Kitu ambacho kinaniumiza kwa sasa ni kwamba baba yangu hajayaona mafanikio yangu aliyonitabiria, lakini mama yangu anayaona, kaka zangu wanayaona pamoja na mtoto wangu wa kwanza anayaona, naweza kusema baba alifariki akiwa na umri mdogo miaka 52,” alisema Ronaldo.

‘My family see, my mum, my brothers, even my old son, but my father, he didn’t see nothing, and it was… he died young.’

Miongoni mwa mafanikio ambaye baba wa Ronaldo amefariki bila ya kuyaona ni pamoja na mataji matano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, tuzo tano za mchezaji bora wa dunia wa Ballon d’Or, ubingwa wa Euro 2016 na mataji mengine mengi pamoja na watoto wanne wa Ronaldo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here