23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Ronaldo akwepa kifungo Ligi ya Mabingwa

TURIN, HISPANIA

MSHAMBULIAJI wa Juventus, Cristiano Ronaldo, amekwepa kifungo cha kukosa kushiriki hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, baada ya Chama cha Soka barani Ulaya, UEFA kuweka wazi.

Mchezaji huyo alikuwa anachunguzwa na chama hicho, baada ya Atletico Madrid kupeleka malalamiko juu yake.


Ronaldo alikuwa analalamikiwa kutokana na aina ya ushangiliaji wake katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Atletico Madrid, ambako alifunga mabao matatu peke yake na kuifanya timu hiyo isonge hatua ya robo fainali.


Baada ya kufunga bao la tatu, Ronaldo alishangilia kwa aina ambayo ilikuwa inatafsiri kuwa ni utovu wa nidhamu, hasa kwa kuwanyanyasa wapinzani wake, kitendo ambacho kiliwafanya Atletico Madrid wapeleke malalamiko kwa chama cha soka.


Aina ya ushangiliaji huo pia ilifanywa na Kocha wa Atletico Madrid, Diego Simeone, katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 bora ambapo Atletico ilifanikiwa kushinda mabao 2-0, kabla ya huo wa marudiano ambapo Juventus walishinda mabao 3-0, lakini kocha huyo alitakiwa kulipa faini ya Euro 20,000.


Hata hivyo, mbali na Ronaldo kukwepa kifungo cha kukosa mchezo wa robo fainali, UEFA imemchukulia hatua mchezaji huyo kwa kumtaka alipe Euro 20,000, ambazo ni zaidi ya Sh milioni 53 za Tanzania.


Kutokana na adhabu hiyo, Ronaldo atakuwa huru kushiriki mchezo unaofuata wa robo fainali dhidi Ajax, ikiwa ni kuelekea kutwaa taji la nne la michuano hiyo mfululizo endapo atafanikiwa kuchukua msimu huu akiwa na Juventus.


Mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid aliweza kuingia kwenye historia ya kutwaa taji hilo mara tatu mfululizo akiwa na Madrid, kabla ya kujiunga na Juventus mwishoni mwa msimu uliopita.


Tangu amejiunga na Juventus, mchezaji huyo hadi sasa amecheza jumla ya michezo 36 kwenye michuano mbalimbali na kufanikiwa kufunga jumla ya mabao 24.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles