27.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 26, 2022

Ronaldo akitua, Sterling anaondoka

ENDAPO Manchester City watamsajili Cristiano Ronaldo, basi winga wake raia wa England, Raheem Sterling, ataondoka Etihad, kwa mujibu wa mwandishi wa habari za michezo nchini Italia, Fabrizio Romano.

Ronaldo anahusishwa na Man City, ikielezwa kuwa nahodha huyo wa timu ya taifa ya Ureno amemwambia wakala wake ahakikishe wanaondoka Juventus kipindi hiki cha usajili wa kiangazi.

Licha ya Sterling kuifungia Man City mabao mabao 115 katika mechi 294, timu hiyo italazimika kumuuza ili kuepuka kuvunja sheria ya Nidhamu ya Utumizi wa Fedha (Financial Fair Play).

Hii si mara ya kwanza kwa mchezaji huyo kuhusishwa na mlango wa kutokea kwani wakati fulani alitajwa kuwindwa na Tottenham.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,044FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles