25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

RONALDO AANDAA NYUMBA YA BIL 13/- KWA WATOTO MAPACHA

MADRID, HISPANIA


MWANAMITINDO maarufu nchini Hispania, Georgina Rodriquez ambaye ni mchumba wa mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya Taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo, anatarajia kujifungua watoto mapacha.

Gazeti la The Sun limeripoti kuwa, mchezaji huyo ameweka wazi kwamba ameandaa nyumba yenye thamani ya Sh bilioni 13 kwa ajili ya kufikia watoto hao na pia ameweka vito mbalimbali vya thamani kwa ajili yao.

Ronaldo ambaye kwa sasa ana mtoto mmoja wa kiume anayejulikana kwa jina la Cristiano Jr, ujio wa watoto hao utaongeza ukubwa wa familia yake lakini kwa mchumba wake huyo mwenye umri wa miaka 23 itakuwa ndio watoto wake wa kwanza.

Kupitia akaunti ya Instagram, Georgina amedai kuwa familia hiyo kwa sasa ipo katika furaha kubwa ikiwa inatarajia kupata watoto hao wawili. “Muda mfupi ujao familia itakuwa kubwa na Cristiano Jr. anatarajia wadogo zake wawili, tuna furaha mno,” aliandika Georgina.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles