Romeo amtaka Bow Wow asistaafu muziki

bow-wow

NEW YORK, MAREKANI

NI wiki moja sasa tangu nyota wa muziki nchini Marekani, Shad Moss maarufu Lil Bow Wow, atangaze kustaafu muziki.

Kutokana na hilo, rapa Romeo Miller, maarufu kwa jina la Lil Romeo, ameibuka na kumtaka msanii huyo asistaafu aendelee na muziki.

Wawili hao walikuwa marafiki tangu wakiwa na umri mdogo, walifanya muziki na kuteka idadi kubwa ya vijana walioupenda muziki sana lakini baadaye walitofautiana kwa madai kwamba walichonganishwa na vyombo vya habari.

Hata hivyo, baada ya kukaa kwa muda mrefu bila mazungumzo, Lil Romeo ameshindwa kuzuia hisia zake juu ya kauli ya Bow Wow kutangaza kustaafu.

“Sidhani kama amefanya maamuzi sahihi, ulimwengu wa muziki bado unamhitaji, hivyo ni vizuri akabadili maamuzi yake. Nilianza muziki nikiwa na umri mdogo na Bow Wow ndio chanzo kwa kuwa alianza muziki akiwa na umri mdogo pia, hivyo alikuwa rafiki yangu mkubwa lakini vyombo vya habari vilitugombanisha, ila bado ni rafiki yangu,” aliandika Lil Romeo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here