25.2 C
Dar es Salaam
Monday, August 15, 2022

ROBO FAINALI CAF:SIMBA YAPEWA TP MAZEMBE

SOSTHENES NYONI-DAR ES SALAAM

SIMBA imepangwa kuumana na TP Mazembe ya DRC  katika mchezo wa  hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambao pia wanafahamika kama Wekundu wa Msimbani, wataanzia nyumbani, Uwanja wa Taifa, Dar es Dar  es Salaam Aprili 4.

Droo ya hatua hiyo ya robo fainali iliyohusisha timu nane, ilichezeshwa jana usiku Makao Makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), jijini Cairo, Misri.

Timu nyingine zilizoingia katika droo hiyo ni  Horoya ya Guinea itakayoumana na Wydad  Casablanca ya Morocco, Constantine ya Algeria itakayopepetana na mabingwa watetezi wa michuano hiyo, Esperance ya Tunisia na  Mamelody Sundown ya Afrika Kusini itakayooneshana umwamba na Al Ahly.

Mshindi kati ya Mazembe na Simba atafuzu nusu fainali na kukutana na mbabe kati ya Constantine na Esperance, wakati mshindi kati ya Mamelod Sundowns na Al Ahly atapambana na mshindi kati ya Wydad Casablanca na Horoya.

Mara ya mwisho Simba na Mazembe zilikutana raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2011. Mchezo wa kwanza Wekundu hao walilala mabao 3-1 jijini Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) kabla ya kufungwa tena mabao 3-2 nyumbani Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Simba ilifuzu hatua ya robo fainali baada ya kuichapa AS Vita mabao 2-1 katika mchezo wa mwisho hatua ya makundi uliofanyika, Uwanja wa Taifa Dar es Salaam Jumamosi iliyopita.

Simba ilimaliza nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi D ikiwa na pointi 9, nyuma ya Al Ahly ya Misri iliyomaliza vinara na pointi 10.

Kwa upande wa Mazembe, ilianzia raundi ya kwanza kwa kucheza na Zesco United ya Zambia, ambapo mchezo wa kwanza ilishinda bao 1-0 nyumbani, kabla ya kulazimisha sare ya bao 1-1 ugenini na kutinga hatua ya makundi kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-1.

 Timu hiyo ilipangwa katika kundi C na timu za Constantine, Club African ya Tunisa na Ismailia ya Misri.

Mazembe ilizindua kampeni zake kwa kuichapa Ismaily mabao 2-0 nyumbani, ikichapwa mabao 3-0 ugenini na Constatine, ikahitimisha michezo ya mkondo wa kwanza kwa kuifumua Club African mabao 8-0.

Ilianza mkondo wa pili kwa kurudiana na Club African na kulazimisha suluhu, ikitoka sare ya bao 1-1 na Ismailia ugenini, kabla ya kumaliza kwa kuilaza Constantine mabao 2-0 nyumbani.

Katika michezo hiyo minane, Mazembe ilishinda mechi nne nyumbani na moja ugenini, huku pia ikipoteza mchezo mmoja ugenini na kutoka sare miwili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,763FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles