25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

ROBINHO JELA MIAKA TISA KWA KUBAKA

MILAN, Italia

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Manchester City na Real Madrid, Robson de Souza ‘Robinho’, amehukumiwa kifungo cha miaka tisa jela baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka msichana raia wa Albania Januari, 2013.

Ripoti kutoka nchini Italia zinaeleza kwamba, Robinho, akiwa na wenzake watano, walihusishwa na kumvamia na kumbaka msichana huyo mwenye umri wa miaka 23 katika klabu ya usiku ya jijini Milan.Tukio hilo ambalo mchezaji huyo alisisitiza hakuwa sehemu hiyo, lilitokea wakati nyota huyo mwenye umri wa miaka 33 akicheza timu ya AC Milan, baada ya kuondoka katika klabu ya Manchester City mwaka 2010.Robinho, ambaye sasa anacheza timu ya Atletico Mineiro ya Brazil, kwa mujibu wa mwanasheria wake hakuwa na hatia na hakuonekana katika mahakama yoyote ya Kaskazini mwa Italia wakati hukumu hiyo ikisomwa.

Hata hivyo, Robinho inadaiwa kuwa ana haki ya kukata rufaa kupinga hukumu hiyo kama anaona anapaswa kufanya hivyo.

Mbrazil huyo alitumia miaka minne kucheza Ligi Kuu Italia, Serie A, akicheza zaidi ya mechi 100 kabla ya kuhamia Ligi Kuu ya China mwaka 2015. Mshambuliaji huyo alivunja rekodi ya usajili ya Manchester City kwa kusajiliwa kwa pauni milioni 32 Septemba, 2008.

Robinho alikuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa kwa fedha nyingi wakati klabu hiyo ikiwa chini ya tajiri wa mafuta, Sheikh Mansour, lakini alicheza mechi 53 katika miezi 18 aliyokuwa kwenye klabu hiyo.

Akiwa kinda, nyota huyo pia alicheza Real Madrid, ambako alitumia misimu mitatu kabla ya kuhamia Ligi Kuu England.

Lakini si mara ya kwanza kwa Robinho kukutwa na kesi ya ubakaji kwani mwaka 2009 mshambuliaji huyo alikumbwa na kashfa kama hiyo baada ya kudaiwa kumbaka mwanafunzi wa chuo cha Leeds nchini Uingereza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles