23.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 27, 2021

RIYAMA: BILA MILIONI NNE HAPANA

NA ESTHER GEORGE


NGULI wa filamu Tanzania, Riyama Ally, amefunguka na kuweka wazi kuwa hawezi kucheza filamu ya kitajiri bila kulipwa Sh milioni nne.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Riyama alisema kiwango chake cha malipo kinatokana na filamu na vipande anavyopewa kucheza, hivyo hawezi kucheza filamu ya maisha ya kifahari bila kulipwa Sh milioni nne kutokana na ugumu wa kuigiza maisha hayo.

“Watu wanafikiri kucheza filamu za maisha ya kifahari ni rahisi, kwangu mimi ni kazi ngumu kwa sababu kuna mambo mengi ya kujiandaa ikiwamo mabadiliko ya mavazi, nywele na vitu vingine ndiyo mana nataka Sh milioni nne,” alisema Riyama.

Aliongeza kuwa filamu zake za mazingira ya uswahilini anacheza kwa Sh millioni mbili hadi tatu inategemea na vipande(Scene) vingapi atakavyopewa kutokana na kutokuwapo mambo mengi ya kugharamia.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
163,314FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles