27.5 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

RITA WAPOKEA MGOGORO WA ANGLIKANA

KAIMU Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Emmy Hudson
KAIMU Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Emmy Hudson

Na ASHA BANI –Dar es Salaam

KAIMU Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Emmy Hudson, amesema wamepokea malalamiko kutoka uongozi wa Kanisa la Angikana kuhusu mgogoro unaofukuta na wanaendelea kuufanyia kazi.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Emmy  alisema wapo katika hatua ya mwisho ya kufanya uchunguzi, kisha kutoa msimamo wao.

Hivi karibuni Katibu Mkuu Kanisa la Anglikana Tanzania, Johnson Chinyong’ole, alitangaza kumvua uaskofu wa Dayosisi ya Dar es Salaam, Dk. Valentine Mokiwa kutokana na kukabiliwa na tuhuma za kuingia mikataba mibovu na matumizi mabaya ya fedha za kanisa makosa yanayoangukia kuvunja sheria za nchi.

Hatua ya kumvua uaskofu Dk. Mokiwa ilizua mtafaruku na msuguano ndani ya kanisa hilo na hadi sasa hakujatulia.

Wakati katibu huyo akimvua uaskofu Dk. Mokiwa, alieleza kufuata sheria zote ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa msajili wa vyama ambaye ndiye anayesajili makanisa, ofisi za Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) kwa kuchukua hatua za kisheria.

Alitaja sheria alizovunja Dk. Mokiwa ni ya Miunganiko ya Wadhamini sura ya 318, Sheria ya Ardhi namba 4 ya 1999 na Sheria ya Mipango Miji sura ya 355 kwa kuruhusu mabadiliko ya matumizi ya ardhi katika shamba la kanisa lililopo Mtoni Buza na eneo la Kanisa la Mtakatifu Mariam Kurasini.

Alisema katika mashtaka 10 anayokabiliwa nayo, shtaka la tatu ni la ubadhirifu wa mali za kanisa ambalo limesababisha Serikali kuingilia kati.

Katika mgogoro wa kiwanja cha kanisa uliopo Yombo Buza, Manispaa ya Temeke tayari wamiliki wa Lamada Hoteli & Apartment wamemwandikia barua ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke kuomba kupimwa na kuhakiki upya mipaka ya eneo la Buza Kanisani.

Kiwanja hicho ndicho ambacho pia kimemuhukumu Dk. Mokiwa na kumfanya kukiri kosa namba tatu la ufujaji wa mali za kanisa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles