24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

RITA kutoa vyeti vya kuzaliwa Maonesho Sabasaba

Asha Bani, Dar es Salaam

Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA), utatoa elimu na huduma mbalimbali zinazotolewa na taasisi hiyo ikiwamo vyeti vya kuzaliwa katika Maonyesho ya biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yatakayoanza kesho katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam.

Meneja Masoko na Mawasiliano wa RITA, Josephat Kimaro amesema mbali na kusajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa pia wakala utatoa ushauri wa kisheria bure kuhusu masuala ya kuandika wosia na mirathi.

“Pia tutapokea maoni, maswali, ushauri na mapendekezo kuhusu huduma za Wakala,” amesema.

Kimaro amesema RITA imekuwa ikishiriki maonesho hayo kila mwaka ambapo mwaka jana RITA ilishiriki na kutoa huduma kwa zaidi ya wananchi 5,524 ambao walisajiliwa na kupata vyeti vya kuzaliwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles