27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

RIPOTI YAFICHUA MADUDU MAFUTA YA KULA BANDARINI

Na MWANDISHI WETU


RAIS Dk. John Magufuli, amemaliza mzozo wa mafuta ya  kula yaliyokuwa yamezuiliwa bandarini huku akabaini madudu ikiwamo udanganyifu wa wafanyabiashara na upungufu wa sheria aliosema yawezekana ulichangiwa na uzembe wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Wakati awali ilidaiwa kuwa mafuta hayo yote yalikuwa ghafi, timu ya wataalamu iliyofanya uchunguzi wa kimaabara kwenye matanki 43 yenye tani 105,630 za mafuta na kubaini kuwa kati ya matanki hayo, 7 yana na mafuta yaliyoboreshwa (refined oil), 14 yana na mafuta yaliyoboreshwa kiasi (semi refined oil), 4 yana ni mafuta ya kutengenezea sabuni (Refined Stearin) na 18 ni mafuta ghafi (crude oil).

Baada ya kupokea ripoti hiyo ya timu ya wataalamu iliyoongozwa na  Profesa Joseph Buchweishaija, Rais Magufuli aliagiza Mamlaka ya Mapato (TRA), kutoza kodi zote zinazostahili na kisha kuruhusu mafuta hayo  yaliyohifadhiwa katika matanki ya Kurasini, kusambazwa kwa walaji.

Matokeo ya ripoti hiyo yameonyesha tofauti na taarifa zilizowasilishwa TRA na kampuni za uagizaji wa mafuta za Vegetable Oil Terminal (VOT), Tanzania Liquid Storage (TLS) na East Coast Oils and Fats Limited (EC) ambazo zilionyesha sehemu kubwa ya mafuta hayo ni ghafi ambayo hutozwa kodi asilimia 10, imebainika kuwa kuna kiasi kikubwa cha mafuta yasiyo ghafi na ambayo yanapaswa kutozwa kodi asilimia 25.

Kwa habari zaidi jipatie nakala ya gazeti la MTANZANIA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles