26.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Ripoti ya PPRA yakataliwa kesi ya vigogo Rahco

Kulwa Mzee -Dar es salaam

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imegoma kupokea ripoti ya ukaguzi iliyotolewa na Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma, Dk. Laurence Shirima, katika kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili vigogo wa Kampuni Hodhi ya Mali za Reli (Rahco) kwa sababu muhuri wa moto hausomeki.

Uamuzi huo mdogo wa mahakama ulitolewa jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, baada ya kupitia hoja za mawakili wa pande zote mbili waliokuwa wakibishania kupokelewa kwa kielelezo hicho.

Ripoti hiyo ya ukaguzi pamoja na mambo mengine ilikuwa ikionyesha mchakato ulivyokwenda wakati wa kuipitisha kampuni ya Rothschild kama mshauri wa mradi wa uimarishaji wa reli ya kati

Washtakiwa katika kesi hiyo ni aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Rahco, Benhadard Tito, Mwanasheria wa Rahco, Emmanuel Massawe na mfanyabiashara ambaye pia ni mwakilishi wa kampuni ya Rothschild (South Africa) Proprietary Limited, Kanji Mwinyijuma.

Hakimu Simba alisema kapitia hoja zilizowasilishwa na Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Maghela Ndimbo akiomba kielelezo hicho kipokelewe na hoja za Wakili Peter Kibatala na Jeremiah Ntobesya waliokuwa wakipinga kwa sababu kina mapungufu.

Alisema nyaraka hiyo imegongwa muhuri wa moto ambao hausomeki, haijulikani nyaraka inatoka wapi, muhuri unatakiwa kugongwa kila kurasa lakini hata ulipogongwa hausomeki.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,608FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles