26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 27, 2021

RIPOTI YA BOT YAONYESHA KUPANDA BEI YA MAHINDI


 

Na Tobias Nsungwe – Dar es Salaam

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imeotoa ripoti ya hali ya uchumi inayoishia mwezi Machi, mwaka huu huku ikionyesha ongezeko kubwa la bei ya vyakula.

Ripoti hiyo imeonyesha kupanda kwa mfumuko wa bei za vyakula kutoka asilimia 5.2 mwezi Januari hadi asilimia 5.5 Februari, mwaka huu.

Kwamba hali hiyo imesababisha kupanda kwa bei za nafaka, hasa mahindi, unga wa mahindi, ndizi, maharage sambamba na vinywaji baridi.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kiwango cha mfumuko wa bei kwa mwaka kwa vyakula na vinywaji visivyo na kilevi ambazo ni bidhaa zinazokusanya walaji wengi zaidi, kilipanda zaidi ya kiwango cha kawaida cha mfumuko wa bei.

 Kwa mtindo wa ripoti ya mwezi hadi mwezi, mfumuko wa bei ulikuwa ni ailimia moja kwa mwezi Februari mwaka huu, ikilinganishwa na asilimia 0.7 ya Februari mwaka jana.

Taarifa ya BoT pia imesema kiwango cha kukua kwa mfumuko wa bei kwa vyakula na vinywaji visivyo na kileo ni asilimia 8.7 mwezi Februari toka asilimia 7.6 ya mwezi Januari mwaka huu.

Kwa kufuata ripoti ya mwezi hadi mwezi, kiwango hicho kilikuwa ni asilimia 2.3 mwezi Februari mwaka huu, ukilinganisha na asilimia 1.2 mwezi Februari mwaka jana.

Viwango vya mfumuko wa bei kwa vitu visivyo vyakula, ilikuwa ni asilimia 3.6 hadi mwisho wa mwezi Februari mwaka huu kama ilivyokuwa mwezi uliotangulia.

Kwa msingi wa mwezi hadi mwezi, kiwango cha mfumuko wa bei kwa vitu visivyo vyakula ilikuwa ni asilimia 0.4 mwezi Februari mwaka huu kama ilivyokuwa mwezi kama huo mwaka jana.

Mfumuko wa bei kwa nishati na mafuta kulipanda hadi asilimia 12.3 kufikia mwezi Februari mwaka huu toka asilimia 11.5 mwezi Januari mwaka huu.

 Katika ripoti ya mwezi hadi mwezi, kiwango kilikuwa asilimia 2.1 mwezi Februari mwaka huu ukilinganisha na asilimia 1.4 mwezi Januari mwaka jana.

Ripoti hiyo imesema pia kuwa katika ripoti ya miezi 12 ya mfumuko wa bei kwa bidhaa zote ukiacha chakula na nishati, ulipungua kwa asilimia 2.2 mwezi Februari mwaka huu kutoka asilimia 2.3 ya mwezi Januari mwaka huu.

Kwa ripoti ya mwezi kwa mwezi, kiwango cha mfumuko wa bei kilikuwa ni asilimia 0.1 mwezi Februari mwaka huu ukilinganisha na asilimia 0.2 mwezi Februari mwaka jana.

Ripoti ya BoT imekuja siku chache baada ya baadhi ya wabunge kulalamikia kuwapo kwa tishio la njaa nchini.

Hali hiyo ilijitokeza bungeni wiki iliyopita wakati wabunge hao walipoanza kuomba mwongozo kwa Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
163,371FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles