31.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

RIPOTI: Tanzania ina mabilionea 99, trilionea mmoja

MASHIRIKA YA HABARI YA KIMATAIFA

RIPOTI mpya ya benki ya AfrAsia imeonyesha kuwa Tanzania sasa ina mabilionea 99, na trilionea mmoja.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya  mwaka 2019 kuhusu utajiri barani Afrika iliochapishwa mwezi Septemba na benki ya AfrAsia, hadi kufikia mwaka jana Tanzania ikitajwa kuwa na Pato la Taifa la dola bilioni 57, imeelezwa ilikuwa na watu wenye utajiri wa hali ya juu  ‘High Net Wealth Individuals’ (HNWI) 2,400.

Hivyo,Tanzania inashika nafasi ya pili nyuma ya Kenya kwa idadi ya watu watu  wenye utajiri mkubwa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kenya inaongoza Afrika Mashariki ikiwa na mabilionea 356.

Mabilionea hao 99 wanaoishi Tanzania wanaiweka nchi kwenye nafasi ya tisa katika orodha ya matajiri barani Afrika.

Ripoti inaonyesha kuwa matajiri hao kila mmoja anamiliki mali au ukwasi wenye thamani ya zaidi ya dola milioni 10 (ambayo ukiibadilisha kwenda shilingi ya kitanzania kwa kikokotoo cha 1USD=2,299.95 TZS  inakuwa ni sawa  na 22,999,485,496.42  au kwa kwa lugha rahisi shilingi bilioni 22)

Aidha ripoti hiyo imebainisha kuwa Tanzania ina tajiri mmoja wa dola bilioni moja (ambayo kwa shilingi za kitanzania ni sawa na Trilioni 2).

Ripoti hiyo ambayo inajulikana kama ‘The Africa Wealth report for 2019’  iliyotolewa na benki hiyo ambayo chimbuko lake ni nchini Mauritius imeiweka Afrika Kusini katika nafasi ya kwanza ikiwa na mabilionea 2,169.

Nchi ya Misri (932), Nigeria (531), Ethiopia (154) Uganda (67) na Rwanda (30).

Hata hivyo ripoti hiyo haikutaja jina la bilionea yeyote wala aina ya mali wanazomiliki zaidi tu ya kutaja idadi.

Shirika la Utangazaji la Uingereza limeinukuu ripoti hiyo ikiitaja miji mikuu inayoongoza kwa utajiri.

Kwa upande wa miji mikuu, mji wa Nairobi unaongoza ukiwa na utajiri wa dola bilioni 49 mbele ya mji wa Dar es salaam ambao umeorodheshwa wa 11 na una utajiri wa dola bilioni 24.

Mji mkuu wa Uganda Kampala una utajiri wa dola bilioni 16 huku Addis Ababa ukiwa na utajiri wa dola bilioni 14.

Kulingana na ripoti hiyo mabilionea wa Afrika ni asilimia 16 pekee ya idadi ya mabilionea wote duniani, huku Afrika ikiwa na silimia moja pekee ya utajiri wote duniani.

Utajiri unaomilikiwa na bara hilo ni dola trilioni 2.2 kwa jumla ambapo asilimia 42 ya utajiri huo unalimikiwa na watu wenye utajiri wa kiwango cha juu au HNWIs.

Kwa ujumla mtu mwenye mapato ya kiwango cha kadri anayeishi Afrika ana mali inayogharimu dola 1,900.

Ripoti hiyo inasema kwamba kuna matajiri 140,000 wanaoishi barani Afrika kila mmoja wao akiwa na mali yenye thamani ya dola milioni 10.

Vilevile kwa mujibu wa ripoti hiyo kuna takriban mamilionea 6,900 wanaoishi Afrika kila mmoja akiwa na mali yenye thamani ya dola milioni 10 ama zaidi mbali na mabilionea wanaopimwa kwa kiwango cha dola ambao ni 23 kila mmoja wao akiwa na mali yenye thamani ya dola bilioni moja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles