31.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 11, 2024

Contact us: [email protected]

Rihanna: Naweza kubadilisha maisha ya Chris Brown

RihannaNEY YORK, MAREKANI

MSANII wa muziki nchini Marekani, Robyn Fenty ‘Rihanna’, amesema kuwa yeye ni mtu pekee anayeweza kumbadilisha, Chris Brown.

Awali wawili hao walikuwa wapenzi, walipoachana Chris akadondokea kwa Karrueche Tran, hata hivyo hakudumu naye baada ya Chris kuletewa mtoto na mpenzi wake wa zamani, Nia Guzman.

Kutokana na kuyumba huku katika mapenzi, Rihanna ameshindwa kuzuia hisia zake na kusema kuwa yeye ndiye mwanamke pekee anayeweza kumbadilisha msanii huyo.

“Nilimzoea sana Chris, nilikuwa kama mlinzi wa mambo yake mengi tofauti na msichana yeyote ambaye atatoka na msanii huyo. Mpaka sasa ninaona kuwa wanashindwa lakini mimi ni msichana wa pekee ambaye ninaweza kuyabadilisha maisha ya msanii huyo.

“Kwa sasa sina uhusiano mzuri na Chris kwa kuwa hatuongei, lakini siwezi kumchukia na nitaendelea kuyalinda maisha yake mpaka mwisho wa maisha yangu. Sio marafiki kwa sasa lakini sio maadui,” alisema Rihanna.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles