Rihanna alizwa na mashabiki

0
1936

NEW YORK, MAREKANI

STAA wa muziki wa Pop nchini Marekani, Rihanna Fenty, mwishoni mwa wiki iliyopita alilizwa na mshabiki wake wanaodai kwamba, msanii huyo amekuwa kimya sana bila kutoa wimbo mpya.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, mrembo huyo aliposti picha yake huku akiwa anatoa machozi na kudai kwamba anaumizwa na kauli za mashabiki.

“Ni kweli nimekuwa kimya sana lakini si bure kuna kazi zipo studio hivyo mashabiki wasiwe na wasiwasi, nimejikuta nikitokwa na machozi kuona jinsi gani mashabiki wangu wananihitaji,” aliandika.

Mrembo huyo mbali ya kufanya muziki, lakini pia ni mfanyabiashara mkubwa wa vifaa vyake vya urembo, hivyo kwa sasa anaonekana kuwa bize na biashara hiyo kuliko muziki na ndio maana mashabiki wake wamekuwa wakihoji.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here