22 C
Dar es Salaam
Friday, August 12, 2022

Ridhiwani awaangukia Dawasa kukamilisha mradi wa maji jimboni kwake

Tunu Nassor, Dar es Salaam

Mbunge wa Chalinze mkoani Pwani, Ridhiwani Kikwete, ameiomba Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) kukamilisha haraka mradi wa maji jimboni humo kwa kuwa wananchi wake wana shida kubwa ya maji.

Akizungumza na waandishi wa habari alipotembelea Kiwanda cha kutengenea mabomba ya chuma (Tanzania Steel Pipes) leo Ijumaa Machi 29, mwaka huu Ridhiwani amesema wananchi wa jimboni kwake wamekuwa wakitumia maji yasiyofaa kwa muda mrefu.

“Wananchi wangu wanachangia kunywa maji na wanyama jambo baya ambalo halijawahi kutokea cha msingi muwe na huruma kwani wananchi wamesubiri huduma hiyo kwa muda,” amesema Ridhiwani.

Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa Dawasa, Aaron Joseph, amesema mabomba ya kusafirishia maji umbali wa kilomita 3.7 yamezalishwa na kiwanda cha TPS kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo.

“Mkataba wa uagizaji viungio vya mabomba umesainiwa kati ya Dawasa na kampuni ya M/S Shanxi na kazi itaanza April 2019 na kukamilika ndani ya miezi minane,” amesema Joseph.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,504FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles