30.9 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

RICK ROSS KUTIKISA KENYA

NAIROBI, KENYA


HATIMAYE rapa Rick Rose kutoka nchini Marekani, amethibitisha kuwa atawasili nchini Kenya mwishoni mwa mwezi ujao kwa ajili ya tamasha la NRG Wave.

Tamasha hilo linatarajia kufanyika Aprili 28, katika Ukumbi wa Carnivore Grounds, hivyo amewataka mashabiki kuwa tayari kwa ujio wa msanii huyo.

Msanii huyo amekuwa akihusishwa kutaka kutua nchini humo kwa ajili ya matamasha mbalimbali, lakini haikuwezekana ila sasa msanii huyo ameweka wazi kuwa yupo tayari kuwapagawisha mashabiki wake Afrika Mashariki.

Staa huyo ataungana na mwanamitindo maarufu nchini Kenya, Huddah Monroe ambaye ni balozi wa kinywaji cha Luc Belaire, ikiwa Afrika Mashariki wawakilishi wake ni Diamond Platnumz kutoka Tanzania pamoja na mrembo huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles