RICK ROSS AREJEA KWA KISHINDO JUKWAANI

0
731

LOS ANGELES, MAREKANIMWANAMUZIKI wa hip hop wa Marekani, Rick Ross, amerejea kwa kishindo katika shughuli zake za kawaida baada ya juzi kufanya tamasha kwa mara ya kwanza katika ukumbi wa Light uliopo mjini Las Vegas, Marekani.

Mapema mwezi huu Rick Ross alidondoka ghafla na kuwahishwa hospitali akidaiwa kuwa na tatizo la moyo lililompata akiwa nyumbani kwake.

Katika tamasha lake, Rick Ross maarufu kama ‘Da Boss’, aliwaeleza mashabiki wake kuwa yupo fiti kuendelea na kazi.

Baada ya kuimba nyimbo chache Da Boss aliomba polisi wamwachie huru rafiki yake kipenzi Meek Mill ambaye anashikiliwa na Jeshi la Polisi la Marekani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here