Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital
KUNDI maarufu la muziki wa Kizazi Kipya kutoka nchini Kenya, Sauti Sol limeachia video ya muziki inayokwenda kwa jina la “Rhumba Japani” wakiwa na Bensoul, Xenia, Nviiri The Storyteller, Okello Max na NHP.
Sauti Sol inachukua mashabiki lukuki ulimwenguni kutokana na uzoefu wao kwenye sanaa ya Pop na video ya muziki yenye vionjo vya kupendeza na kusherehekea, vinavyotokana na uzoefu mkubwa waliopata kutokana na kazi zao nyingi zilizopita.
Hiyo ni furaha ya kusherehekea kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu walipoachia albamu yao ya tano ‘Midnight Train’.
Mbali na video yao hiyo ya “Rhumba Japani”, kundi hilo ni mabalozi wa simu aina ya Infinix Note Pro10, ambayo ilizinduliwa hivi karibuni.
Wakielezea maana ya jina la kibao chao hicho, “Rhumba Japan” mmoja wa wasanii wanaounda kundi hilo anasema: “Kuna bendi moja ya Kikongo inaitwa Rhumba Japan. Tulikuwa tukienda kuwatazama wakicheza kwenye baa moja, Nairobi. Tulikuwa tunakwenda baada ya mazoezi yetu kukwepa ule muda wa foleni.
“Na baada ya muda huo tulielekea nyumbani tukiwa tumepata kitu, wakati wa kusubiri foleni ya magari barabarani ipungue. Kwetu ilikuwa kitu muhimu sana kwa nyakati hizo. Hatuwezi kusahau.”