25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Republican wampinga Trump kwa kutaka kusogeza uchaguzi

 WASHINGTON, MAREKANI

VIONGOZI wa juu wa chama cha Republicans wamempinga Rais Donald Trump wa Marekani kwa kutaka kusogeza mbele Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo kwa hofu ya kufanyika udanganyifu.

Kiongozi wa waliowengi katika baraza la Seneti, Mitch McConnell na kiongozi wa wachache wa Baraza la Wawakilishi, Kevin McCarthy wote wamepinga hoja hiyo. 

Wamesema Trump hana mamlaka ya kuahirisha uchaguzi.

Kwamba hatua yeyote ya kuahirisha uchaguzi itaidhinishwa na Bunge.

McCarthy amesisitiza kuwa “ haijawahi kutokea katika historia eti uchaguzi usifanyike ni lazima twende mbele na uchaguzi wetu,”.

Mfuasi mkubwa wa Trump, ambaye pia ni Seneta Lindsay Graham naye amesema kupeleka mbele uchaguzi si wazo sawa sawa.

Juzi Rais Trump alipendekeza uchaguzi wa urais utakaofanyika Novemba uahirishwe akidai kuongezeka kwa upigaji kura kwa njia ya posta kunaweza kusababisha udanganyifu na matokeo yasiyo sahihi.

Kuna ushahidi mdogo wa madai ya Trump lakini kwa kipindi kirefu amekuwa akipinga upigaji kura kwa njia ya posta ambao anadai unaweza kusababisha udanganyifu.

Majimbo ya Marekani yanataka upigaji kura kwa njia ya posta kufanywa kuwa rahisi zaidi kwasababu ya wasiwasi wa matatizo ya kiafya kutokana na janga la corona.

Katika ujumbe wake kwa njia ya Tweeter, Trump alisema kupiga kura kwa njia ya posta kutafanya uchaguzi wa Novemba kuwa usio sahihi na wenye udanganyifu mkubwa katika historia ya nchi hiyo na aibu kubwa kwa Marekani. Alisema hivyo bila kutoa ushahidi wowote kwamba kupiga kura kwa njia ya posta kama inavyofahamika Marekani, kutahatarisha uchaguzi kuingiliwa na nchi za kigeni.

“Wanazungumza kuhusu uchaguzi kuingiliwa na nchi za kigeni lakini wanajua kwamba upigaji kura kwa njia ya posta ni njia rahisi ya nchi za kigeni kuuingilia,” alisema.

Mapema mwezi huu, majimbo sita ya Marekani yalikuwa yanapanga kufanya uchaguzi wa Novemba kwa njia ya posta.

Majimbo hayo ni California, Utah, Hawaii, Colorado, Oregon naWashington.

Majimbo hayo yatatuma kura moja kwa moja kwa njia ya posta kwa wapiga kura wote waliosajiliwa, na baada ya hapo zitarejeshwa tena au kuwasilishwa siku ya kupiga kura – ingawa kupiga kura moja kwa moja bado kutakuwepo kwa wachache ambao hali italazimu kufanya hivyo.

Chini ya uchaguzi wa urais, Trump hana mamlaka yoyote ya kuahirisha uchaguzi yeye binafsi na tukio kama hilo ni lazima liidhinishwe na bunge.

Juni, New York iliruhusu raia kupiga kura kwa njia ya posta katika uchaguzi wa awali wa chama cha Democratic kumtafuta mgombea wa kupeperusha bendera ya chama hicho. 

Lakini kuhesabiwa kwa kura kulicheleweshwa na hadi kufikia sasa matokeo bado hayajulikani.

 Vyombo vya habari vya eneo vimesema kwamba pia kuna wasiwasi kuwa wapiga kura wengi hawatahesabiwa kwasababu hawakujazwa vizuri au pengine hawana alama zinazoonesha kwamba kura zao zilitumwa kabla ya siku ya upigaji kura kufikia ukomo wake rasmi.

Hata hivyo kuna majimbo mengi ambayo kwa muda mrefu sasa yamekuwa yakipiga kura kwa njia ya posta.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles