24.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

REPSSI Tanzania wamkumbuka baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere


Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Wakati ikiwa siku ya pili, ya Jukwaa la Kimataifa la Msaada wa Kisaikolojia (PSS FORUM), Mkurugenzi Wa REPSSI Tanzania, Edwick Mapalala ametumia nafasi hiyo kumuelezea baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

Mwenyekiti wa Bodi ya REPSSI Tanzania, Jeanne Ndyetambura(wakwanza kushoto) akifuatilia kongamano hilo pamoja na wajumbe wengine.

Regional Psychosocial Support Initiative (REPSSI) ni shirika lenye makao makuu nchini Afrika Kusini, likijihusisha kwenye masuala ya malezi, makuzi na saikolojia hasa ya watoto katika nchi zaidi ya 13, Tanzania ikiwemo.

Katika siku ya pili ya Jukwaa la Kimataifa la shirika hilo, Mapalala amesema Tanzania inakila sababu ya kujivunia uwepo wa amani iliyoasisiwa na baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere.

“Kuna nchi siku moja nilikuwa huko, ikatokea kuna binti amevamiwa na kibaka, tukaogopa kusaidia lakini kuna walinzi pembeni tuliwaomba wamsaidie, wakauliza kwani yule binti kabila gani?” amesema na kuongeza;

“Tanzania hatuulizani kuhusu ukabila, tuna amani, unajua thamani ya kitu ukiwa nacho huwezi kuiona. Utaiona pale ukipoteza kitu hicho,” amesema.

Afisa miradi msaidizi wa REPSSI Tanzania, Phinehas Mussai akifuatilia kongamano hilo kwa njia ya mtandao.

Jukwaa la Msaada wa Kisaikolojia linafanyika wakati dunia ikikubwa na changamoto ya UVIKO – 19 jambo lililosababisha liendeshwe kwa njia ya mtandao.

Wadau wa masuala ya watoto na msaada wa kisaikolojia wakiwemo maafisa ustawi wa jamii kutoka Tanzania, wanashiriki jukwaa hilo wakiwa katika Hoteli ya Ramada, jijini Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles