25 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 8, 2021

Rehema Simfukwe mbioni kukamilisha albamu

Christopher Msekena

MWIMBAJI mahiri wa Injili nchini, Rehema Simfukwe, ameweka wazi kuwa yupo katika hatua za mwisho za kutoa albamu yake mpya hivyo wapenzi wa muziki huo wajiandae kuipokea.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Rehema ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo Corona wenye lengo la kumwomba Mungu aingilie kati janga la ugonjwa wa corona, alisema albamu yake itakuwa na jumla ya nyimbo nane.

“Nikiwa najiandaa kutoa albamu yangu ambayo bado sijaipa jina niliachia wimbo unaitwa Nisaidie Bwana ambao umekuwa msaada kwa wapendwa wengi na lilipoingia janga la corona nikaachia video ya wimbo Corona ambao haupo kwenye albamu,” alisema Rehema.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,540FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles