30.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Regency yaanza kambi uchunguzi wa magoti

Mwandishi Wetu -Dar es Salaam

MADAKTARI bingwa kutoka nchini India wameanza kuwafanyia uchunguzi na upasuaji wagonjwa wenye matatizo ya magoti na viungo hapa nchini.

Huduma ya uchunguzi na upasuaji inafanywa katika  Hospitali ya Regency ambayo inashirikiana na Hospitali ya HCG Group ya India kwa muda wa siku tatu kuanzia leo.

Taarifa iliyotolewa na hospitali hiyo kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana, ilisema wataalamu hao wataendesha kambi ya siku tatu kuanzia leo kwa watu wenye matatizo ya viungo kama magoti na mgongo.

Iliwataja wataalamu watakaoendesha kambi hiyo ni Dk. Yuvraj Lakum ambaye ni daktari bingwa wa nyonga na magoti akisaidiana na Dk. Kuastubh Chauhan.

Taarifa hiyo ilisema wataalamu hao watatumia mbinu mpya kwenye upasuaji ambayo ni kukata sehemu ndogo kuhakikisha mgonjwa anapona mapema.

Ilisema ujio wa wataalamu hao utapunguza gharama za wagonjwa kwenda nje ya nchi kufuata tiba hiyo.

“Katika jitihada za kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda kufuata matibabu nje ya nchi na kuokoa fedha nyingi za kigeni ambazo zimekuwa zikitumika, tumeona ni vyema kuita mara kwa mara mtaalamu huyu kufanya upasuaji hapa Dar,” ilisema taarifa hiyo.

IIisema ujio wa wataalamu hao umekuwa ukisaidia kuwapa ujuzi wataalamu wa ndani ili wawe na utaalamu wa kufanya upasuaji wa aina hiyo wao wenyewe.

Taarifa hiyo ilisema mpango wa kuita madaktari hao bingwa wa magoti na viungo umekuwa ukiratibiwa na Hospitali ya Regency kwa kushirikiana na Hospitali ya HCG Multi-Specialty iliyoko Ahmedabad nchini India.

 “ Hii ni fursa ya kipekee kwa watanzania wenye matatizo kama haya kuchangamkia fursa hii kwani badala ya kwenda nje na kutumia gharama kubwa kusafiri na wasaidizi wao kwenda nje ya nchi sasa wanafanyiwa upasuaji hapa hapa nchini,” ilisema taarifa hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles