25.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 12, 2024

Contact us: [email protected]

Real Madrid yamtimua Lopetegui

Madrid, Hispania


Klabu ya Real Madrid imemfuta kazi kocha wake , Julen Lopetegui (52) baada ya miezi minne na nusu ya kudumu klabuni hapo.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya kupoteza kwenye mchezo wa El Clasico dhidi ya wapinzani wao wa jadi Barcelona ambao ni mchezo wa tano kufungwa katika michezo sita ya ligi kuu nchini humo waliyocheza.

Mhispania huyo alichukua mikoba kutoka kwa Zinedine Zidane. Huu ni mwanzo mbaya zaidi wa Real Madrid tangu walipofanya hivyo mwaka 2001-2002.

Madrid ambayo inashikilia rekodi ya kutwaa ubingwa wa klabu bingwa ulaya mara tatu mfululizo, ipo nafasi ya tisa kwenye msimamo wa La Liga.

Mikoba ya Lopetegui, itarithiwa na kocha wa timu ya vijana ya Madrid, Santiago Solari (42) aliyewahi kuwa mchezaji bora Madrid miaka ya nyuma.

Lopetegui, alishiriki mazoezi na wachezaji siku ya Jumatatu ingawa adhma yake ya kusalia klabuni hapo imefutwa na kikao cha dharura cha bodi ya timu hiyo kilichokaa siku ya Jumatatu jioni.

Madrid ina alama sita juu ya timu zilizo kwenye mstari wa kushuka daraja na alama saba nyuma ya vinara Fc Barcelona.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles