25.1 C
Dar es Salaam
Saturday, December 9, 2023

Contact us: [email protected]

Real Madrid kumnyatia Harry Kane

kaneMADRID, Hispania

KLABU ya Real Madrid ipo katika maandalizi ya kutafuta mbadala wa mshambuliaji wao, Cristiano Ronaldo, anayetarajia kuhama timu hiyo kwa kuanza mazungumzo na mshambuliaji wa klabu ya Tottenham Hotspur, Harry Kane.

Madrid wanatazama namna ya kupata huduma ya mshambuliaji huyo kwa muda mrefu ikiwa ni maandalizi ya kukijenga kikosi hicho baada ya kuonekana zama za Ronaldo kuishia.

Klabu hiyo imedaiwa kuwa katika utaratibu wa kumnasa mchezaji huyo tangu mwaka mmoja uliopita wakati Kane alipofanikiwa kufunga mabao saba kati ya michezo nane ikiwa pamoja na mabao mawili aliyofunga katika mechi dhidi ya Chelsea.

Uhusiano wa Madrid na klabu hiyo umeongezeka kuliko ilivyokuwa wakati aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo, Daniel Levy, ilipofanya usajili wa Luka Modric pamoja na Gareth Bale.

Ingawa klabu hiyo ipo makini katika kufuatilia maendeleo ya mchezaji huyo zaidi ya mwaka mmoja, hakuna uwezekano wa kumsajili mchezaji huyo mwezi huu kwa kuwa Spurs inajiandaa kumfanya kuwa moja kati ya usajili mkubwa kufanyika Ulaya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles