Renatha Kipaka, Bukoba
KAMATI Maalum ya Ushauri ya Maendeleo ya Mkoa wa Kagera (RCC) imepenekeza kuwa zitakuwepo athari nane ikiwamo kudorola kwa uchumi endapo wilaya mbili za Ngara na Biharamulo zitachukuliwa kwa ajili ya kuanzishwa Mkoa mpya wa Chato.
Athari nyingine ni kupungua kwa mchango kiuchumi kwa mkoa na Taifa, kudhoofisha umoja wa Wanakagera kiuchumi, kisiasa, kijamii, kuongezeka gharama za serikali, upungufu wa fursa za ajira na ufinyu wa ardhi
Akizungumza katika kikao cha kamati hiyo, Novemba 23,2021 kilichofanyika kwenye ofisi za Mkoa wa Kagera, Katibu Tawala Msaidizi wa mkoa huo, David Ryamboka, amesema maeneo yaliyopendekezwa ndiyo yenye rasilimali nyingi kama madini, ardhi nzuri kwa kilimo, ufugaji, utalii, hivyo itapunguza mchango wa Mkoa wa Kagera kitaifa katika nyanja tajwa.
Amesema malighafi za viwanda mfano zao la kahawa aina ya arabika inayozalishwa Ngara kwa wingi.
Kwa upande wa faida iliyotajwa ni faida moja imetajwa ya kusogeza huduma za kijamii karibu pekee.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Charles Mbuge ambaye alikuwa Mwenyekiti wa kikao hicho, amewataka wajumbe wa kikao kujadili kwa hekima na busara juu ya kumega wilaya mbili za Ngara na Biharamlo kwenda Chato na kuwa wachambue faida na hasara za kumegwa kwa wilaya hizo kutoka Kagera.