29.7 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

RC WA ARUSHA MRISHO GAMBO KUWA SHAHIDI WA KWANZA KESI YA LEMA

Lema na mkeweMkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo anatarajiwa kuwa Shahidi wa kwanza katika kesi namba 351 ya mwaka jana inayomkabili Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na mke wake Neema Lema.

Mbele ya Hakimu Nestory Barro wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, katika kesi hiyo ya uchochezi Lema na mkewe wanadaiwa kutoa kauli za kukashifu dhidi ya Gambo ambapo leo watuhumiwa hao wamesomewa hoja za awali za shitaka linalowabili.

Lema alikuwa akitetewa na Wakili John Mallya na Sheck Mfinanga,huku Serikali ikiwakilishwa na Wakili Alice Mtenga.

Alice alidai Lema na mkewe walituma ujumbe mfupi wa sms, “Karibu tutakudhibiti kama uarabuni wanavyodhibiti mashoga”, ujumbe unaodaiwa wa kumuudhi na kumuumiza Gambo.

Baada ya kusomewa hoja hizo watuhumiwa hao walikana kutenda kosa hilo ambapo pia Wakili Mallya alitoa notisi ya pingamizi la mdomo la kuipinga hati ya mashitaka iliyowashitaki watuhumiwa hao kutokana na kuwa na mapungufu ya kisheria na kuwa baadaye wataiomba Mahakama iitupilie mbali hati hiyo.

Hakimu Barro aliahirisha kesi hiyo hadi Februari 3 mwaka huu,hoja za pingamizi hilo zitakapowasilishwa kwa njia ya mdomo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles